Lucas Digne Akubali Masharti Binafsi na Aston Villa

Lucas Digne amekubali masharti binafsi na Aston Villa huku beki huyo wa Everton akikaribia kuhamia kikosi cha Steven Gerrard kwa kima cha pauni milioni 25 baada yakuripotiwa kuafikiana na klabu hiyo.

Lucas Digne Akubali Masharti Binafsi na Aston Villa

Aston Villa wanatumaini kubwa la kumpata beki huyo wa pembeni ndani ya wiki na bosii wa Everton alithibitisha wiki iliyopita kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa  anataka kusepa Goodison Park.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alisaini kandarasi mpya mwezi Februari, ambayo ingedumu hadi 2025, na inasemekana kuwa anapokea pauni 120,000 kwa wiki.

Chelsea na Newcastle zote zimekuwa zilihusishwa na beki huyo wa kushoto, lakini Aston Villa wanaonekana kushinda katika kinyang’anyiro cha kuwania saini yake.

Hii ni nia nyingine ya Steven Gerrard na Villa siku chache baada ya kutangaza kumsajili kwa mkopo Philippe Coutinho.

Nyota huyo wa zamani wa Liverpool atajiunga na Villa akitokea Barcelona hadi mwisho wa msimu huu.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe