Brendan Aapa Kubaki Leicester

Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers hana nia ya kuondoka King Power Stadium licha ya timu yake hiyo kuanza vibaya msimu huu, ambapo mpaka sasa wapo mkiani mwa EPL baada ya kupata alama moja tuu kwenye mechi zao sita walizocheza ikiwa ni pamoja na kupoteza mechi tano mfululizo.

 

Brendan Aapa Kuipigania Leicester

Mchambuzi wa Skysports Jammie Carragher alipendekeza kuwa wiki iliyopitakuwa raia huyo wa Ireland Kaskazini  ilikuwa inatosha lakini kocha huyo wa zamani wa Liverpool alitupilia mbali madai hayo mara moja.

Brendan(49), alisema:“Sio hivyo hata kidogo, napenda kuwa hapa. Pengine napata maswali mengi ambayo yananichosha kuwa mkweli. “Lakini,  Hapana ni muda mrefu zaidi ambao nimekaa kwenye klabu na ninapenda kuwa hapa na nitapambana hadi pumzi ya mwisho kubaki na kuifanya timu kuwa bora tuwezavyo kwa kile tulichonacho”

Baada ya kuiongoza Leicester Brendan alichukua kombe la FA kwa mara ya kwanza katika historia, miezi 16 pekee, mwisho wa msimu uliopita kumaliza katika nafasi ya nane ilikuwa ni mdororo kwenye kampeni za awali.

 

Brendan Aapa Kuipigania Leicester

Wasiwasi ulikuzwa zaidi baada ya msimu wa joto wa kutokuwa na shughuli katika soko la usajili, ikichochewa na wamiliki wa klabu kukaza mikoba kutokana na hasara zinazohusiana na janga, ingawa Mbweha hao walikazania kuwashikilia wachezaji wao muhimu kama vile James Maddison, Harvey Barnes na Youri Tielemans, ambapo Fofana alikwenda Chelsea huku wao wakifanikiwa kumsajili  mchezaji mmoja tuu ambaye ni  Wout Faes kutoka Reims.

 

Brendan Aapa Kuipigania Leicester

Baada ya kuahirishwa kwa mechi za ligi za Uingereza kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth wa pili, mechi ya ligi kuu ya Leicester itakuwa ni dhidi ya Tottenham Spurs mnamo Septemba 17.

 

Acha ujumbe