Bondia Maarufu kwa sasa nchini Tanzania Karim Mandonga amevunja ukimya na kuzungumzia pambano la bondia mwenzake Hassan Mwakinyo ambalo lilipiganwa Septemba 3, 2023 Jijini Liverpool.

Katika pambano hilo Mwakinyo alipotezo kwa TKO dhidi ya Liam Smith katika raundi ya nne ya mchezo kwa kushindwa kuendelea kutokana na kile alichokitaja yeye “viatu vilikuwa vinambana na kupelekea yeye kupata maumivu ya mguu”.

Mandonga Ampasua Mwakinyo

Kwa mujibu wa Dodoma_tv Mandonga alisema kuwa Mwakinyo angeomba watanzania wamchangie pesa ya kununua viatu isinge shindikana, ila kaamua tu kuliabisha taifa.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Official Dodoma Tv (@dodoma_tv)

Katika sehemu ya Mahojiano hayo Mandonga alisema kwamba “Mwakinyo ameonesha udhaifu mkubwa, hakuna bondia wa mchongo kama yule. Apiganie heshima ya Tanzania. Bondia anapaswa afie ulingoni, azimie au apelekwe hospital. Mwakinyo aache kupigana mechi za mchongo” Alisema Mandonga.

Mandonga Ampasua Mwakinyo

Karim aliyejizolea umaarufu wake kwa hivi karibuni baada ya kudundwa na Hassan Kaoneka kwa TKO na kumfanya afikishe mapambano 4 kupoteza kwa KO na kushinda pambano moja tu kati ya matano aliyowahi kupigana, ukiachilia mbali yale mapambano yake mawili lile la sensa na lile alilopigana Bagamoyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa