Kwa misimu mitatu iliyopita, nne bora kwenye Laliga imekuwa ikitabirika kwa kiasi fulani. Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid ameingia kwenye nafasi tatu za juu, huku Sevilla akiambulia nafasi ya nne na kufuzu kwa Champions League.

 

Laliga: Hili ni Pambano la 4 Jipya?

Ingawa inawezekana kuwa hivyo msimu wa 2022/2023, mwanzo mbaya wa vijana wa Julen Lopetegui umewafanya wakiambulia pointi moja kutoka kwenye michezo yao minne ya kwanza waliyocheza huku wakishikilia nafasi ya 17 kwenye msimamo.

Kwa kutabirika, mbio za mapema za Laliga zimezifanya Madrid na Barcelona kuweka kasi, ingawa timu zingine mbili ambazo zimeanza vizuri zitakutana Estadio Benito Villamarin siku ya Jumapili ambapo itakuwa ni Real Bets dhidi ya Villareal.

 

Laliga: Hili ni Pambano la 4 Jipya?

Betis wameonyesha mwendelezo thabiti misimu ya hivi karibuni, baada ya kumaliza nafasi ya 15 msimu wa 2019/2020, na baada ya kuwa na Manuel Pellegrin walipanda hadi nafasi ya sita mwaka uliofuata na kisha nafasi ya tano  msimu uliopita pamoja na kubeba Copa Del Rey.

Athari za Pellegrin zimekuwa za kustaajabisha hapo Laliga  kutokana na timu hiyo kuendelea kufanya vizuri  na kupigania mpaka nafasi ya kucheza michuano ya Europa. Betis mpaka sasa ndani ya mechi nne alizocheza ameshinda tatu na amepoteza moja, Wakati kwa upande wa Villareal ameshinda mechi tatu na ametoa sare moja kwenye ligi hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa