Brentford Wachukizwa na Ubaguzi kwa Mshambuliaji Ivan Toney

Klabu ya Brentford inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza imelaani kitendo cha kibaguzi ambacho amefanyiwa mshambuliaji wao wa kutumainiwa Ivan Toney baada ya mchezo wao dhidi ya Arsenal.

Ivan Toney ambaye alifunga bao la kusawazisha dhidi ya klabu ya Arsenal katika dimba la Emirates hapo jana, Amekumbana vitendo vya kibaguzi dhidi yake kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram na hii inakua sio mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kukumbana na hali hii.BrentfordKupitia taarifa yao waliyoiweka kwenye mitandao ya kijamii klabu ya Brentford waliandika “Tumechukizwa na kuhuzunishwa kua Ivan Toney amelazimika kukabiliana na hili tena,Hatutavumilia na tutafanya kila tuwezalo kuwafuata wanaohusika”

Klabu ya Brentford waliendelea kueleza kua nyota huyo alikabiliwa na ubaguzi wa rangi na mtuhumiwa alipelekwa mahakamani hivo anakabiliana na ambacho alikifanya, Klabu hiyo inataka kuhakikisha na ambae amehusika wakati huu wanampata ili kukomesha vitendo vya kibaguzi ambavyo vimekua vikiendelea kwa wachezaji mbalimbali wenye asili ya Afrika.BrentfordKlabu ya Brentford imekua moja ya klabu ambayo imekua ikitoa ushirikiano kwa wachezaji wake ambao wamekua wakipitia vitendo vya ubaguzi ikiwa inaonesha utofauti na vilabu vingine ambavyo mara nyingi vimekua havichukuliia kwa uzito suala la ubaguzi kwa wachezaji wao.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.