Kiongozi wa klabu ya Brighton Hove and Albion Paul Barber amesema ana imani kua klabu hiyo ina uwezekano mkubwa wa kumbakiza kiungo wake raia wa Argentina Mac Allister.

Mac Allister ambaye alikua kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kilichotwaa ubingwa wa dunia siku ya jumapili, Kiungo huyo ameanza kunyemelewa na vilabu mabalimbali barani ulaya kutokana na uwezo mkubwa ambao ameuonesha kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka huu.brightonMac Allister ambaye amefanikiwa kuanza kwenye michezo sita kati ya saba ambayo Argentina wamecheza kwenye kombe la dunia ikiwemo mchezo wa fainali ambapo alipiga pasi ya bao la pili kwa Angel Di Maria, Huku kiongozi wa Brighton Paul Bareber yeye amesema hatarajii kiungo huyo kuondoka klabuni hapo hivi karibuni.

Paul Barber ambaye ni mkurugenzi katika klabu ya Brighton ameweka wazi kua kwasasa wanafanya mazungumzo na kiungo Mac Allister huku akisema wamekutana na baba yake kiungo huyo mara kadhaa kwajili ya kujadili mkataba mpya wa kiungo huyo.brightonMac Allister mwenye umri wa miaka 23 amekua akionesha kiwango kizuri ndani ya klabu ya Brighton ndani ya ligi kuu ya Uingereza, Lakini kiwango chake bora kabisa kwenye michuano ya kombe la dunia kimekua gumzo na kufanya timu mbalimbali kuanza kumtolea macho.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa