Kwanza wacha niihusie nafsi yangu kabla sijahusia nafsi ya mwingine kwenye yale yote mema ikiwemo kumtamkia mema binadamu mwenzako, naombeni Kumbukumbu la Torati kwa kalamu yangu nilipigia mstari maneno matakafitu
Rejea Marko 9:5 inasema “Mwalimu, ni vizuri sisi kuwapo hapa, Basi, afadhali tujenge vibanda vitatu, Kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Elia”, nilipenda sana kusikia hadithi hii juu ya ujenzi wa vibanda pale Mlimani, nami nataka nimsafirishe Bwalya mpaka nyuma ya muda kumpa historia ya vibanda vitatu
Najua nimeanza na gubu sana, sijakukaribisha Tanzania najua nimevunja sheria zetu za ujamaa aliotuachia Mwalimu Nyerere, pengine imetokana na haraka zangu nyingi kutaka kumaliza hadithi yangu kwako, najua miguu ni ya dhahabu na akili ya computer, najua hilo
Naomba tupande kwenye milima ya Uluguru Morogoro mji kasoro bahari, kibanda cha kwanza wala sio cha Elia, kumbuka tumerudi kwenye maisha ya kawaida, kibanda hiki aliishi Patrick Mutesa Mafisango, usisahau
Moja Kati ya Viungo bora kutokea nchini, ile juu ni jezi yake namba 32, vile chini ni viatu vyake vya Adidas, pale pembeni ni maua na mashada ya mashabiki wa Simba, waliohusudu soka lake kuliko chochote
Kibanda hiki cha Mafisango hakina mtu kwasasa, kama uonavyo Mjumbe wa Mtaa mlangoni, mwenye kibanda chake ametangulia mbele za haki, ila ndani kuna vitabu na Kila kitu kwa ajili yako kurithi
Ikiwapendeza Simba watakupa funguo ufungue, ukutane na bidii, kipaji na roho Ngumu, ikiwapendeza lakini, wao wenyewe wenye Simba yao sio Mimi, uyakutayo ni wewe kuamua sasa
Rally naomba tupite kwenye kibanda hicho tusogee kwenye kibanda cha Pili, nadhani umekiona kilivyojitenga, hapa anaishi Mtoto wa Msimbazi, kipenzi chao aliefika hapa akiwa na miaka 19 tu, hakutumia pesa kuishinda mioyo yao, bali miguu yake kwenye viwanja vya Vita
Alitokwa jasho hata kama mvua inanyesha, angepiga kelele kuwaamsha wenzake, kuna muda aliamua mechi kupitia miguu yake, anaitwa Emmanuel Okwi The Prince of Simba, najua unashangaa taa inawaka na walinzi wapo nje wanalinda hatuwezi kuingia ndani kumradhi
Itaendelea..
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.


felister
kumbukumbu nzuri
Nasra
Gud
Caroline
Kweli hi ni hadithi ya vibanda vitatu.na inahusiana kabisa
Fatina mfigi
Gud
Zeiyana
Mashujaa hao watazidi kukumbukwa na ndio walio hifanya simba hionekane Leo hii r i p okwi
r i p mafisango
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri Sana Bwalya
Adelta
Good 👍
Shafii
Gud news.
aisha
Hadithi ya vibanda vitatu inasisimua ajabu ahsanteni sana
Saupha mohamed
Good news
Mwajumah
Kweli hadithi ya vibanda vitatu ila mashujaa hao watazidi kukumbukwa
Tatu
Hadithi nzuri inatuelisha na kutufundisha
Shani
Bwalya simba ni kama hawataelew kabumbu lako ila mida itaongea
Hopemwaikuka
Nmetoka kapa
Elika
Safi sana
Gabriel
Mashujaa hao watazidi kukumbukwa
Amiri Kayera
Safii
Rehema
Fresh
Ernest
Makala nzuri mwandishi umeweza kututeka hisia zetu kwenye kusoma neno moja adi lingine, Kazi nzuri sana
Sadick
Mafisango ni kiungo wa level nyingine kabisa ambae hawezi kusahaulika ndani msimbazi#meridianbettz
Issa
Mtu hatari sana huyu pale msimbaz
David Pere
Kweli hadithi ya vibanda vitatu ila mashujaa hao watazidi kukumbukwa
Rose kapinga
Wakumbukwe daima
Sabrina
Akumbukwe alivyokua shujaa
magdalena
imekaa vizuri sana hii hadithi
Dorophina
Ni mashujaa wa nchi kumbu kumbu zao zimeandikwana haziwezi kusahaulika kabisa
Povel
Bwalya mtu sahihi pale Msimbazi