Arsenal wameenda vyumbani kupumzika, kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu haswa. Fulham wamekuwa wakorofi, wamewadhibiti Arsenal vilivyo. Arsenal wanatembelea ‘mtungi’, pumzi imewakatikia, wanasubiri tu kurejea ili wakafungwe. Si kwa moto waliowashiwa kipindi cha kwanza na Fulham.
Wachezaji wote wakiwa wamekaa chini wanasubiri maelezo ya Arsene Wenger aliingia Patrice Vierra, moja kwa moja akamfuata Nikolas Anelka akamuambia “Tungeweza kutoka tunaongoza, ila kwa ujinga wako umekosa nafasi ambayo hata mwanangu wa miaka mitano angepata. Halafu haukabi kabisa, unazurura tu uwanjani. Kama unapenda kutembea sana usingekuja Arsenal, ungeenda kuwa muigizaji wa ufukweni na mkeo”.
Nikolas Anelka akavimba, akamuambia Vieirra “Wewe unanikaripia kama nani? Hicho kitambaa tu cha unahodha ndio kinakupa kiburi? Kama unadhani ni rahisi, njoo wewe ucheze namba tisa”. Hapo ndipo Vieirra akavaa ule ukichaa wake halisi. Akashusha bukta yake akabaki uchi kisha akamuambia “Mimi ni nahodha hapa lakini kabla ya unahodha mimi ni mwanaume. Shusha macho yako unitazame vizuri. Ndiyo maana nafanya kazi za kiume pale katikati ya uwanja. Sirembui kama wewe. Acha upumbavu, turudi tukaipiganie Arsenal. Mimi na wewe ni mali ya hii klabu.”
Arsene Wenger alimuita Vieira pembeni akampa tano akimpongeza kwa nzuri ya unahodha anayofanya. Licha ya yeye kuwa kocha, hakuwa na uwezo wa kufoka kama Vieirra. Robert Pires anasema ilifika kipindi wakawa wanamuita Vierra Tyson , hakuna mchezaji aliyekuwa na uwezo wa kukohoa mbele yake. Akisema kimya kila mchezaji anafunga mdomo.
Nimekikumbuka hiki kisa baada ya kuiona picha ya Mesut Ozil akiwa na kitambaa cha unahodha. Hivi ni kweli Ozil huyuhuyu amewahi kuwa captain wa timu?
Nimekumbuka pia Patrice Vierra alivoondoka Arsenal. Aliona imani ya kocha kwake imepungua. Isitoshe Cesc Fabregas alishaandaliwa vema kumrithi. Akaona hana cha kusubiri, japo ilikuwa ngumu, akafanya maamuzi akaondoka. Nimekumbuka alivoondoka Patrick Vieira baada ya kutokumuona Ozil kwenye kikosi cha kwanza. Hata benchi siku hizi hayupo, vijana wameaminiwa zaidi. Anasubiri nini zaidi?
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.
felister
makala nzuri
Nasra
Asantee kwa makala
Caroline
Dah jmn hichi kisa ni atari.kavua nguo uwanjani
Zeiyana
Arsenal ya Wenger ndio ilikua ya moto sasa hivi akuna kitu
Lydia Emmanuel Magoti
Arsenal ilikuwa kipindi hicho asaivi Amna timu humo
Antony Luseno
Ozil kama ni mpira kashacheza sana bora arudi nyumbani ujerumani astaafie kwao
Adelta
Makala nzuri Sana
Shafii
Makala imesimama sana patrick viera alikua kiungo matata Sana.
aisha
Arsenal ilikua zamani sasa ivi haina maajabu kabisa
Saupha mohamed
Good news
Khadija
Asante kwa nakala
Sadick
Patrick Viera ilikuwa shughuli nyingine pale ktkt ya uwanja na ndivyo Nahodha unatakiwa kuwa hivyo#meridianbettz
Mwajumah
Arsenal ya zaman ndio ilikua mpango mzima lakn asaivi hamna kitu
Tatu
Kipindi cha nyuma arsenal ilikuwa moto
Agness
Makala nzuri
Shani
Ozil asepe the gunners hana chake
Hopemwaikuka
Uamuz upo kwake
Elika
Maamuzi yapo kwake
Gabriel
Ozil kama ni mpira kashacheza sana
Amiri Kayera
Ozil kiwango kimeisha
Rehema
Maamuzi yake
Ernest
Tunaweza sema Arsenal watakuwa vizuri sana kipindi hiki lakini Binafsi siwaoni Arsenal kama timu tishio ndani ya EPL
Issa
The gunners mtu kama ozil unamwekaj nje ndio maana wanafeli kweny ubingwa
David Pere
Tunaweza sema Arsenal watakuwa vizuri sana kipindi hiki lakini Binafsi siwaoni Arsenal kama timu tishio ndani ya EPL
Rose kapinga
Vierra kama vierra jembeee
Sabrina
Vierra mtu mbaya
magdalena
wenger alikuwa anajua jinsi ya kuwatumia vizuri wachezaji wake
Dorophina
Patrick alikuwa mchezaji matata sana
Povel
Arsenal ni gari la mkaa muda wwte linazima lile
Furahav
Habari nzuri.