Mambo ni magumu kunako klabu ya Real Madrid kwenye dirisha la usajili kuelekea msimu ujao. Kwa Carlo Ancelotti, mpatieni Kylian Mbappe au Mohamed Salah, inatosha.
Madrid wanasikilizia sakata la Mbappe na PSG linavyokwenda. Je, ataongeza mkataba au ataondoka kama mchezaji huru ifikapo 2022? Hapa Carlo Ancelotti anacheza mchezo wa pata potea kuelekea msimu ujao.
Madrid hawana wachezaji mahiri kwenye safu ya kushambulia ambao pengine Ancelotti anawaona kama wachezaji wa kutegemea kuelekea msimu ujao. Kwa sababu hii, kocha huyu amemueleza wazi raisi wa Madrid – Florentino Perez kuwa anataka nyota mpya atue Bernabeu kwenye usajili wa majira haya.
Katika hili, Ancelotti amemtaja Mohamed Salah kama mchezaji anayemuhitaji endapo Mbappe itashindikana kutua Madrid wakati huu. Inasemekana Salah ameshawaeleza Liverpool mara kadhaa kuwa anataka kwenda Madrid na pia, mahusiano yake na Jurgen Klopp na baadhi ya wachezaji wa Liverpool sio mazuri kwa sasa.
Linapokuja suala la gharama, Salah hatajwi kama mchezaji wa gharama kubwa akilinganishwa na Mbappe lakini kwa yeyote, Real Madrid lazima wauze wachezaji ili waweze kumsajili mchezaji wa kariba ya Mbappe au Salah.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!
Ernest
Ngoja tuone