Gwiji wa zamani wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza Jamie Carragher amesema kocha wa timu ya taifa ya Uingereza napaswa kua Muingereza.
Baada ya Uingereza kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la dunia kumeibuka mijadala mbalimbali juu nani anapaswa kua kocha mpya wa timu hiyo, Kwani wengi wanaamini kocha wa sasa wa timu hiyo Gareth Southgate hatoshi kwenye uchumba.Katika mjadala mmoja kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter uliokua unazungumzia kocha gani ambaye anafaa kuvaa viatu vya kocha Southgate ndipo gwiji huyo alipojitokeza na kusema kocha timu hiyo anapaswa kua Muingereza.
Jamie Carragher anataka kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza awe raia wa taifa hilo hata ikitokea kocha wasasa Gareth Southgate ameng’atuka basi kocha ajaye wa timu hiyo anapaswa kua raia wa nchi hiyo.Timu ya taifa ya Uingereza imeshawahi kua na makocha kutoka nje ya taifa la Uingereza kama Fabio Capello na Sven Goran Erickson lakini haikuwahi kufika hatua kubwa kwenye michuano mbalimbali mikubwa, Lakini kocha Southgate ambaye ni muingereza amefanikiwa kufika nusu fainali ya kombe la dunia 2018 huku pia akifika fainali ya Euro 2020 hivo kumfanya Jamie Carragher kuamini kocha mzawa anaweza kufanya makubwa kwenye timu hiyo.