Gwiji wa zamani waklabu ya Fc Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani ambaye kwasasa ni mkurugenzi mkuu wa klabu Bayern Munich Oliver Kahn amesema hawatafanya usajili wa golikipa wa Croatia Dominik Livakovic.
Klabu ya Fc Bayern Munich imepata pigo baada ya golikipa wake namba moja Manuel Neurer kufanyiwa upasuaji wa goti na kufanya kukosekana kwa kipindi kizima cha msimu uliobakia, Hivo kufanya watu wengi kufikiri klabu hiyo itaingia sokoni kutafuta golikipa.Klabu ya Fc Bayern Munich kwasasa ina nafasi mbili ambazo ni kuamua kubaki na golikipa wake chaguo la pili Sven Ulreich au kuingia sokoni kutafuta golikipa mwingine ambaye atavaa viatu vya Manuel Neurer kikamilifu kumalizia msimu uliobaki.
Oliver Kahn ameeleza kua hawataingia sokoni kutafuta golikipa mwingine mbadala wa Neurer licha ya kuhusishwa na golikipa anayefanya vizuri kwasasa na timu ya taifa ya Croatia Dominik Livakovic ila gwiji huyo amesema golikipa huyo hayupo kwenye mipango yao.Gwiji Oliver Khan amekiri kua golikipa huyo ni mzuri na mwenye ubora na pia anaelewa namna ambavyo imekua pengo kuumia kwa Neurer, Hivo wanahitahi kutafuta mbadala wa muda lakini Dominik Livakovic hayupo kwenye mipango yao.