Chelsea Bado Wanajipigia Tu

Unaweza kusema bado wanajipigia ndio kauli ambayo unaweza kuitumia kwa klabu ya Chelsea, Kwani leo tena wamepoteza mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Everton.

Chelsea wamejikuta wakipoteza mchezo wa pili mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kupokea kichapo cha mabao mawili kwa bila leo dhidi ya klabu, Hii imekuja baada ya kufungwa na Man United katikakati ya wiki.ChelseaMatajiri hao kutoka jiji la London leo walienda Goodson Park wakihitaji alama tatu ili kuweza kurudisha hali ya kujiamini katika michezo yao ya mbeleni, Lakini mambo yalikua tofauti kwani waliendelea walipoishia.

Everton walionekana na mpango wao wa kila siku kuzuia kwa umakini mkubwa na kufanya mashambulizi ya kushtukiza na mpango wao huo uliwalipa na kufanikiwa kupata mabao mawili katika mchezo huo.ChelseaMabao ya klabu ya Everton yalifungwa na Abdoulaye Doucore pamoja na Lewis Dobbin ambaye alitokea nje, Kwa matokeo hayo klabu ya Chelsea inashuka hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza huku Everton wao wakiendelea kushika nafasi ya 17 wakiwa na alama 13 na ni baada ya kupokonywa alama 10.

Acha ujumbe