Klabu ya Manchester City leo wameona mwezi baada ya kufanikiwa kupata ushindi dhidi ya klabu ya Luton Town katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.
Manchester City baada ya kutopata matokeo ya ushindi katika michezo minne ya ligi kuu ya Uingereza hatimae leo wameweza kuchomoza kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja.Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza walitanguliwa kwa bao moja kipindi cha kwanza na kuonekana kama wataendeleza kilichotokea katika michezo minne iliyopita.
Kipindi cha pili vijana wa Pep Guardiola walikuja kwa kasi wakionekana kuhitaji kusawazisha goli walilotanguliwa, Ambapo dakika ya 62 ya mchezo Bernardo Silva aliisawazishia City goli kabla ya dakika 65 Jack Grealish kufunga bao la ushindi.Manchester City sasa wanafanikiwa kufikisha alama 33 wakikamata nafasi ya nne kwenye ligi kuu ya Uingereza, Huku wakizidiwa kwa alama nne na vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Liverpool wenye alama 37.