Manchester City na Chelsea Hali Tete

Klabu ya Manchester City na Chelsea wako kwenye kipindi kigumu kwasasa baada ya klabu ya Everton kupokonywa alama 10 baada ya kuvunja sheiria za matumizi ya fedha.

Everton wamepokwa alama 10 siku chache zilizopita baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria ya matumizi ya fedha na mamlaka husika nchini Uingereza, Hivo kwasaa matumbo joto yamehamia kwa vilabu hivi viwili.manchester cityManchester City na klabu ya Chelsea walikua wakituhumiwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha na kuvunja sheria zilizowekwa katika ligi hiyo, Hivo kinachisubiriwa kwa vilabu hivo ni kama mamlaka zitakuja na uthibitisho na wao wakutane na rungu la adhabu.

Utaratibu uliokwekwa ni kua klabu yeyote inatakiwa kufanya matumizi kulingana na mapato yanayoingia kwenye klabu hiyo, Hii imekua sheria imekua ikishinda vilabu vingi na kujikuta wanafanya matumizi makubwa kuluko kinachoingia klabuni na kuishia kudanganya.manchester cityKlabu ya Chelsea na Manchester City wao walithumiwa tangu msimu uliomalizika hivo adhabu ya Everton ambayo imetoka siku kadhaa nyuma inaweza kuwarudisha kwenye wasiwasi mkubwa, Kwani wanatambua hawapo salama kabisa kutokana na mashtaka yanayowakabili.

 

 

Acha ujumbe