Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Gabriel Jesus anatarjiwa kurejea katika kikosi cha Arsenal hvi karibuni baada ya kuonekana akifanya mazoezi na wenzake katika timu ya taifa ya Brazil.
Gabriel Jesus alikua kwenye majeraha na kukosa michezo kadhaa ya klabu yake ya Arsenal, Lakini aliitwa kwenye timu ya taifa ya Brazil na leo ameonekana kwenye mazoezi ya pamoja na yuko tayari kutumika kwenye michezo inayofata ya Selecao.Mshambuliaji huyo tangu amejiunga na klabu ya Arsenal msimu uliomalizika amekua akiandamwa na majeraha ya hapa na pale, Ikiwa hata msimu huu pia tayari ameshakubwa na majeraha mara mbili jambo linalomzuia kuonesha ubora wake.
Kikosi cha Brazili kinatarajia kukipiga katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2026 dhidi ya timu ya taifa ya Argentina, Huku mshambuliaji huyo akitarajiwa kua sehemu ya kikosi cha kocha wa timu hiyo Fernando Diniz.Hii ni taarifa nzuri kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal kwani kuumia kwa Gabriel Jesus wiki kadhaa nyuma ni jambo ambalo liliwavunja moyo, Hivo taarifa za mchezaji kuonekana yupo fiti ni wazi kua kocha Mikel Arteta na mashabiki wa klabu hiyo wamefurahia urejeo wa mshambuliaji huyo.