Bruno Fernandes Awachomolea Waarabu

Kiungo wa klabu ya Manchester United na nahodha wa klabu hiyo Bruno Fernandes amekanusha juu ya yeye kujiunga na klabu yeyote inayoshiriki ligi kuu Saudia Arabia kama tetesi zinavyoeleza.

Bruno Fernandes ameweka wazi kua akili yake kwasasa inawaza klabu moja tu na sio kingine ni Manchester United na kueleza yote yanayoskika nje huko ni tetesi tu na hana mpango wa kutimka klabuni hapo.bruno fernandesKiungo huyo amekua akihusishwa na vilabu mbalimbali kutoka nchini Saudia Arabia, Lakini yeye mwenyewe ameweka wazi hana mpango wa kuondoka klabuni hapo.

Kiungo Bruno Fernandes ameonesha kutokufurahishwa pia na tetesi juu yake juu ya kwamba anataka kutimka klabuni hapo na kwenda Saudia, Kwani amesema siku hizi ni rahisi kusambaza taarifa zisizo za kweli lakini yeye anaangalia malengo yake tu ndani ya Man United.

Acha ujumbe