Nahodha na kiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes raia wa kimataifa wa Ureno amefanikiwa kuiokoa Man United leo katika dimba la Craven Cottage mbele Fulham.

Bruno Fernandes mfungaji wa bao pekee lililoipa Man United alama tatu muhimu mbele ya klabu ya Fulham leo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kutoka kupoteza michezo miwili mfululizo.bruno fernandesBaada ya Manchester United kupoteza michezo miwili mfululizo mbele ya Man City wikiendi iliyopita na Newcastle katikati ya wiki hatimaye wanafanikiwa kupata alama tatu mbele ya Fulham.

Klabu ya Fulham ilionekana kucheza vizuri zaidi  na kutengeneza nafasi za kufunga lakini hawakufanikiwa kufunga goli, Huku kwenye upande wa kuzuia pia wakizuia vizuri sana kabla ya nahodha wa klabu ya Man United kuja kufunga bao pekee lililoipa alama tatu klabu hiyo.bruno fernandesBruno Fernandes anafanikiwa kuiokoa Manchester United jioni kabisa baada ya kuonesha juhudi binafsi na kupiga mkwaju dakika ya 90 ya mchezo ulimshinda golikipa Ben Leno na kuipa alama tatu muhimu Man United.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa