Mshambuliaji wa klabu ya Manchester Marcus Rashford inaelezwa atakosekana katika mchezo wa leo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Fulham utakaopigwa katika dimba la Craven Cottage.

Mshambualiaji huyo ametaarifiwa kua na majeraha na hataweza kuwepo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza msimu huu akikosekana katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.rashfordRashford alifanikiwa kusafiri na timu hiyo kuelekea jijini London mapema jana lakini hali imekua tofauti kwani hataweza kucheza leo dhidi ya Fulham, Huku Ten Hag akisema hiyo ni kutokana na mchezaji huyo kutokua sawa.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye alikua na msimu bora msimu uliomalizika, Lakini msimu huu mambo yameonekana kumuendea tofauti kwani mpaka sasa amefunga goli moja tu kwenye ligi kuu ya Uingereza.rashfordTaarifa mbalimbali zinaeleza kua inawezekana Rashford hajapata majeraha kama taarifa ya timu inavyoeleza, Huku wakisema inaweza kocha ameamua kumuacha mchezaji huyo kutokana na kiwango chake kuporomoka.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa