Real Madrid Yakanusha Kufanya Mazungumzo na Mbappe

Klabu ya Real Madrid imetoa taarifa rasmi kukanusha kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga ndani ya klabu ya PSG Kylian Mbappe.

Real Madrid wamesema wameelezwa kua wanafanya mazungumzo na mshambuliaji Kylian Mbappe jambo ambalo wamelikanusha na kusema hawawezi kufanya mazungumzo na mchezaji wa PSG.mbappeMshambuliaji Kylian Mbappe amekua akihusishwa na klabu hiyo kutoka nchini Hispania na taarifa mbalimbali zikieleza ameshaingia makubaliano na mabingwa hao wa muda wote barani ulaya.

Mshambuliaji Mbappe ni msimu wa tatu sasa anahusishwa na kujiunga na Real Madrid, Lakini klabu hiyo imegoma kabisa kufanya mazungumzo na mchezaji huyo ikieleza haifanyi mazungumzo na wachezaji wa timu nyingine.mbappeKlabu hiyo mbali na kukanusha kufanya mazungumzo na Mbappe lakini haijakanusha kua haina nia ya kumsajili Mbappe, Hivo inawezakana klabu hiyo imejaribu kuipiga chenga ya mwili klabu ya PSG ambayo inaweza kuishtaki klabu hiyo kwa kufanya mazungumzo na mchezaji wake akiwa kwenye mkataba.

Acha ujumbe