Manchester City Yaua Doku Akitakata

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kupata alama tatu kwa kishindo baada ya kuibamiza Bournamouth mabao sita kwa moja, Huku winga Jeremy Doku akitakata.

Manchester City wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamepata alama tatu muhimu kwa ushindi wa kishindo mbele ya Bournamouth na kuwafanya kwenda kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.manchester cityMabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza walifanikiwa kuanza mchezo huo kwa kasi ambapo ndani ya kipindi cha kwanza walipata mabao matatu ambayo yaliwapa uongozi wa mchezo huo.

Kipindi cha pili klabu hiyo iliendelea ilipoishia ambapo walifanikiwa kupata mabao mengine matatu, Huku winga Jeremy Doku usajili mpya ndani ya klabu hiyo akitakata kwelikweli baada ya kufunga bao moja na kupika mabao manne.manchester cityMabao ya Manchester City yalifungwa Jeremy Doku, Bernardo Silva mabao mawili, Akanji, Nathan Ake, pamoja na Phil Foden na kuwafanya Man City kufikisha alama 27, Lakini stori kubwa ni uwezo ambao ameuonesha Jeremy Doku katika mchezo wa leo.

 

Acha ujumbe