Manchester City Yaibuka Kidedea Derby Day

Klabu ya Manchester City wamefanikiwa kuibuka kidedea katika mchezo derby kati yao na mahasimu zao klabu ya Manchester United ambapo wamefanikiwa kushinda mabao matatu kwa bila.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Old Trafford ambapo Man United walikua wenyeji wa mchezo, Lakini ni Manchester City ambao walifanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo.Manchester CityMagoli ya Earling Haaland aliyefunga mabao mawili na Phil Foden ndio yaliyoiwezesha Man City kutoa adhabu katika mchezo huo na kuwafanya vijana hao wa Pep Guardiola kusogea mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Vijana wa Pep Guardiola kama kawaida yao walianza mchezo huo kwa kasi wakionekana kutaka kupata bao la mapema katika mchezo huo, Ambapo walifanikiwa baada ya Rasmus Hojlund kumfanyia madhambi kiungo Rodri kwenye eneo la hatari na kusababisha penati ambayo iliwekwa kimiana na Earling Halaand.Manchester CityManchester City walifanikiwa kwenda mapumziko wakiongoza bao moja kwa bila, Huku Man United wakionekana kufikiwa sana na golikipa Onana kuchomoa michomo kadhaa kipindi cha pili ndio Man City waliukamata mchezo kwa kiwango kikubwa na kufanikiwa kuiua mechi kwa mabao mawili ya Haaland na Phil Foden.

Acha ujumbe