Westham Wapasuka Mbele ya Everton

Klabu ya Westham United wakiwa nyumbani wamekubali kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya klabu ya Everton ambao walikua katika nafasi za chini kabisa kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Westham United chini ya kocha David Moyes wanapoteza mchezo wa pili mfulululizo na hiyo baada ya kukubali kichapo cha mabao matatu kwa moja wikiendi iliyopita dhidi ya klabu ya Aston Villa.westhamMchezo huo uliopigwa katika dimba la London ulishuhudua vijana wa David Moyes wakiwa kwenye umiliki wa mpira kwa muda mrefu mbele ya Everton, Lakini hawakuweza kufua dafu kutokana na Everton kuzuia kwa nidhamu ya hali ya juu.

Mchezo huo ulimalizika kipindi cha kwanza kwa sare ya bila kufungana lakini wagonga nyundo wa London wakioneakana kutengeneza nafasi na kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa mbele ya Everton ya kocha Sean Dyche.westhamEverton wao baada kupoteza mchezo wa derby wikiendi iliyomalizika dhidi ya Liverpool, Leo wameamka na kupata matokeo ya ushindi mbele ya Westham United na bao pekee likifungwa na mshambuliaji Dominic Calvert Lewin ambaye amefanikiwa kufunga bao lake la 50 la ligi kuu ya Uingereza.

Acha ujumbe