Xabi Alonso Hapoi na Leverkusen Yake

Kocha wa klabu ya Bayern Leverkusen Xabi Alonso ameendelea alipoishia na hii ni kutokana na mwenendo wa klabu hiyo katika michezo ya klabu hiyo msimu huu.

Xabi Alonso ameiongoza tena Bayern Leverkusen kushinda mchezo tena leo katika ligi kuu ya Ujerumani baada ya kupata ushindi wa mabao matatu kwa mawili wakiwa ugenini mbele ya TSG Hoffenheim.xabi alonsoBayern Leverkusen ambao walipata mabao kipindi cha kwanza huku wenyeji wakiwa hawajapata goli, Lakini kipindi cha pili kilikuja na mabadiliko ambapo Hoffenheim walisawazisha mabao yote mawili na ubao kusomeka 2-2.

 

Bayern Leverkusen walifanikiwa kuongeza bao la tatu na kuweza kujihakikishia alama tatu muhimu katika mchezo huo, Ambapo klabu hiyo imefanikiwa kufikisha 28 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Ujerumani.xabi alonsoBayern Leverkusen ya Xabi Alonso imecheza michezo 10 ya Bundeslifa msimu huu na kushinda michezo 9 na kusuluhu mmoja huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja, Klabu hiyo imecheza michezo 15 kwenye michuano yote na imefanikiwa kushinda 14 na kusuluhu mmoja rekodi bora kabisa msimu huu.

Acha ujumbe