Beki wa kimataifa wa Ureno Goncalo Inacio ameingia kwenye rada za klabu ya Real Madrid huku ikielezwa klabu hiyo inataka kumsajili katika dirisha dogo la mwezi Januari.
Goncalo Inacio mwenye umri wa miaka 22 tu ameingia kwenye rada za klabu ya Real Madrid kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu ya Sporting CP ya nchini Ureno.Beki huyo amekua akifuatiliwa na vilabu kadhaa barani ulaya kutokana na kiwango ambacho anaonesha ndani ya klabu hiyo, Man United nao wametajwa kuwania saini ya beki huyo anaetumia mguu wa kushoto.
Klabu ya Real Madrid kwasasa inamtumia David Alaba kama beki wake wa kati anaetumia mguu wa kushoto, Lakini wanamuona Inacio mwenye miaka 22 kama mbadala sahihi wa Alaba ambaye umri unaendelea kumtupa mkono.Mabingwa hao wa muda wote wa ulaya wamekua wakitafuta mibadala ya wachezaji wao ambao umri umesogea mapema, Kwani kabla beki kitasa Sergio Ramos hajaondoka klabuni hapo klabu hiyo ilimsajili beki Eder Militao kutoka Fc Porto kwajili ya kujiandaa na kuondoka kwa Ramos.