Klabu ya Manchester United leo watashuka dimbani kumenyana na klabu ya Newcastle United katika mchezo wa kombe la EFL raundi ya nne na swali likiwa je Man United watajipata kwa Newcastle leo?

Manchester United ndio watatoa majibu leo kama watajipata au wataendelea kuchezea vichapo kama ambavyo imekua kawaida kwako siku za hivi karibuni, Kwani klabu hiyo mpaka sasa imeshapoteza micheza saba kwenye michuano yote.manchester unitedNewcastle United moja ya vilabu bora kabisa katika ligi kuu ya Uingereza kwasasa na mchezo huu utakua wa kisasi, Kwani Newcastle walipoteza mchezo wa fainali katika kombe hili msimu uliomalizika mbele ya Man United.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuenda kua mgumu tena kwa Man United kwani mpinzani ambae wanaenda kucheza nae yupo kwenye ubora mkubwa, Newcastle ni moja ya timu ambazo zimefunga magoli mengi msimu huu huku Man United wao wakiwa moja ya timu zilizorhusu mabao mengi msimu huu.manchester unitedKlabu ya Manchester United imekua na mfululizo wa matokeo mabaya siku za hivi karibuni, Huku Newcastle wakiwa na matokeo mazuri lakini kwenye mpira wa miguu lolote linawezekana kwani Man United wanaweza kufanikiwa kupata matokeo ya ushindi leo.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa