Chelsea Kuongeza Ukubwa wa Vyumba vya Kubadilishia Nguo

Klabu ya Chelsea imeamrishwa kuongeza ukubwa wa vyumba vya kubadilishia nguo baada ya klabu ya Liverpool kulalamikia kuwa vyumba hivyo ni vidogo.

Klabu za Liverpool, Southampton na Brighton wanaelewa swala hilo baada ya kulalamika mara kadhaa kwa mamlaka husika kuhusu ukubwa wa sehemu hiyo ambayo timu wageni wanatumia .

Chelsea
Vyumba vya timu ya ugenini stamford bridge

Bodi ya ligi imeiamrisha klabu ya Chelsea kufanya maboresho ya vyumba hivyo na kuongeza ukubwa ili kuweza kuamabatana sheria za uviko-19, ili kuweza kuachiana nafasi pindi watakapo kuwa vyumbani kutokana na milipuko inayotokea mara kwa mara kipindi hiki.

Chelsea wameanza kuongezea ukubwa wa vyumba vya kubadilishia nguo kwa kupunguza nafasi sehemu ya mikutano, ambayo wanakutana na waandishi wa habari na kuwa ndogo ili kuweza kuongeza nafasi kwenye vyumba vya timu ng’eni.

Chelsea
Vyumba ya timu ya nyumbani Stamford bridge

Vyumba ambavyo timu ya Chelsea wanavitumia wakiwa kwenye dimba la Stamford bridge ni vikubwa na kisasa, huku kukiwa na vitu vingi vya kuwafanya waweze kuwa na furaha kulinganisha ni mgeni.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe