Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema amemuunga mkono Lionel Messi kung’ara katika klabu ya Paris Saint-Germain kwa kusisitiza kuwa ni ‘suala la muda tu’ kwa Muargentina huyo kuanza kung’aa.
Tangu atue PSGs, Messi amekuwa akikabiliwa na majeraha na amefanikiwa kufumania nyavu mara sita pekee katika mechi 16 alizocheza. Wakati wa mapumziko ya Krismasi, Messi pia alipimwa na kukutwa na COVID-19 nchini Argentina na alizuiliwa kufanya mazoezi binafsi ya kupona kwa zaidi ya mwezi.
“Huwezi kumkosoa mchezaji kama Messi, anayemkosoa, ni mtu ambaye haelewi chochote kuhusu soka kwa kweli!”, Benzema alisema katika mahojiano na kituo cha Ufaransa cha Telefoot.
Messi amekosa mechi tatu katika kipindi chake cha mwezi mmoja akiwa hayupo, wakati huo PSG wameendeleza uongozi wao kileleni mwa Ligue 1.
Messi akitokea benchi dakika ya 63 akichukua nafasi ya Di Maria alihusika katika ushindi wa 4-0 wa PSG dhidi ya Reims siku ya Jumapili akitoa pasi ya goli la tatu lilifungwa na Marco Verratti.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.