Harry Maguire amekuwa akipambana na Manchester United hivi karibuni, na shaka juu ya nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Erik ten Hag, imeripotiwa kuwa imesababisha Chelsea kufanya jitihada za kuinasa saini ya beki huyo.

maguire, Chelsea Wanamuhitaji Harry Maguire, Meridianbet

The Blues tayari wapo kwenye mazungumzo na United, kuhusu uwezekano wa kuondoka kwa Christian Pulisic, na wameuliza kuhusu Maguire katika mpango wa kubadilishana. Tuchel anatamani sana kuimarisha safu ya ulinzi na, ingawa Wesley Fofana ndiye anayepewa kipaumbele Zaidi.

maguire, Chelsea Wanamuhitaji Harry Maguire, Meridianbet

 

Gazeti la The Mirror limeandika kuwa “Thomas Tuchel anatafuta beki mpya na anafahamu kuwa Manchester United wanamtaka Christian Pulisic. Hilo limefungua uwezekano wa Chelsea kumtoa fowadi huyo wa Marekani kwa kubadilishana na beki huyo wa kati wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa