Chelsea Yaipiku Arsenal kwa Mudryk

Klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa Mykhaylo Mudryk kutoka Shakhtar Donetsk ambaye alikuwa akiwindwa na vinara wa Ligi Arsenal kwa muda mrefu.

 

Chelsea Yaipiku Arsenal kwa Mudryk

Mykhaylo Mudryk atagharimu kifurushi cha €100m kwani Chelsea wamekubali masharti yote yanayotakiwa na Shakhtar Donetsk katika mazungumzo ya moja kwa moja leo.

Mudryk, amewasili London usiku wa kuamkia leo huku vipimo vya afya vikiwa vikitarajiwa kufanywa leo hii ili kukamilisha dili hilo pia kwa upande wa mchezaji baada ya saa 24 ili awe mchezaji kamili wa The Blues.

Chelsea Yaipiku Arsenal kwa Mudryk

Mkataba wa Chelsea na mchezaji huyo utatiwa saini baada ya vipimo vya afya kwa miaka saba ijayo, kwa hivyo mpango huo utakuwa halali hadi Juni 2030.

Arsenal wamefanya vyema zaidi kwa kutoa €70m pamoja na €25m na kufikia makubaliano na mchezaji huyo, lakini walitaka kuwa wazi na maono yao, mkakati wao na kutoingia kwenye mapambano dhidi ya The Blues.

Chelsea Yaipiku Arsenal kwa Mudryk

Licha ya kusajiliwa na timu ya hiyo ya Darajani mchezaji huyo timu yake pendwa ilikuwa ni Arsenal, lakini sasa atakuwa ni kijana wa Graham Potter, na leo atakuwa uwanjani kushuhudia mechi ya Chelsea vs Crystal Palace.

Acha ujumbe