Mgombea urais wa Barcelona, Marc Ciria, ameibua gumzo kwa kuweka bango kubwa lenye picha ya nguli wa klabu hiyo Lionel Messi katikati ya jiji, ikiwa ni sehemu ya kampeni zake za kuwania nafasi ya kumrithi rais wa sasa, Joan Laporta.
Bango hilo lina picha maarufu ya Messi akiinua jezi yake ya Barcelona mbele ya mashabiki wa Real Madrid katika dimba la Santiago Bernabeu mwaka 2017, baada ya kufunga bao la ushindi dakika za majeruhi. Ciria ameambatanisha pia kauli mbiu iliyowahi kutumiwa na Laporta katika kampeni zilizopita “Looking forward to seeing you again.”
Uchaguzi wa urais wa Barcelona unatarajiwa kufanyika Machi 15, huku Laporta akionekana kupewa nafasi kubwa ya kushinda na kuendelea na muhula mwingine. Hata hivyo, anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wagombea kadhaa akiwemo Victor Font, pamoja na Xavier Vilajoana, Daniel Juan na William Maddock.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Jina la Messi limekuwa likitajwa mara kwa mara katika kampeni hizi, huku Ciria akisisitiza kuwa kurejea kwa nyota huyo ni jambo la msingi kwa mustakabali wa klabu. Awali aliwahi kusema kuwa Messi ni sura isiyoweza kutenganishwa na Barcelona, akifananisha uhusiano wao na ule wa Michael Jordan na Nike, akimaanisha kuwa unapaswa kuwa wa kimkakati, kibiashara na kiutamaduni kwa manufaa ya klabu.
Kwa upande wake, Victor Font naye ameahidi kuwa simu yake ya kwanza akishinda uchaguzi itakuwa kwa Messi. Hata hivyo, hali ni tofauti kwa Laporta, ambaye inadaiwa uhusiano wake na Messi uliharibika kufuatia kuondoka kwa nyota huyo mwaka 2021.



