Golikipq namba moja wa klabu ya Manchester United David De Gea leo atafanikiwa kuweka rekodi ya kuingia kwenye kumi bora ya wachezaji waliocheza michezo mingi ndani ya klabu hiyo.
Golikipa huyo amekua kwenye kiwango bora kwa muda mrefu ndani ya klabu ya Manchester United huku akifanikiwa kushinda kila taji ndani ya timu hiyo kasoro ligi ya mabingwa barani ulaya, Leo atafanikiwa kucheza mchezo wake wa 510 na kuingia kwenye kumi bora ya wachezaji walioitumikia klabu hiyo michezo mingi.
De Gea leo kama akifanikiwa kuanza mchezo dhidi ya Afc Bournamouth ataungana na magwiji kama Ryan Giggs,Bobby Charlton,Garry Neville, Paul Scholes, Wayne Rooney, pamoja na Denis Irwin ambao wameitumikia klabu hiyo michezo mingi zaidi.
Golikipa huyo ameitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa tangu alipojiunga klabuni hapo mwaka 2011 chini ya kocha Sir Alex Ferguson, Na mpaka sasa bado anaendelea kuonesha ubora mkubwa ndani ya klabu ya Manchester United.
De Gea msimu huu anaonekana kuimarika zaidi chini ya kocha Ten Hag kutokana na namna anavyocheza ndani ya timu hiyo, De gea hajafanikiwa kuruhusu bado tangu mwezi wa nane katika dimba lao la nyumbani Old Trafford ikiwa ni rekodi nzuri kwake na akiendelea kudhihirisha ubora wake.

