Enzo Fernandez Aelezeaa Mustakabali Wake Na Chelsea FC

Kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, ameacha gumzo kubwa baada ya kutoa kauli yenye utata kuhusu hatma yake klabuni kufuatia kipigo kizito dhidi ya Paris Saint-Germain katika UEFA Champions League. Chelsea walitolewa kwa jumla ya mabao 8-2, hali iliyozua maswali mengi kuhusu mustakabali wa baadhi ya nyota wao wakubwa.

Enzo Fernandez Aelezeaa Mustakabali Wake Na Chelsea FC

Baada ya mechi, Enzo alipoulizwa moja kwa moja kuhusu kama ataendelea kubaki Stamford Bridge, hakutoa jibu la uhakika. Alisema bado kuna mechi kadhaa zilizobaki pamoja na FA Cup, na baada ya hapo ndipo ataamua hatma yake. Kauli hiyo imeongeza uvumi, hasa wakati PSG wakiripotiwa kufuatilia hali yake kwa karibu.

Licha ya kushindwa kwa timu, Enzo mwenyewe binafsi amekuwa na msimu mzuri, akichangia mabao 12 na asisti sita katika mechi 45. Hii inaonyesha kuwa bado ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Chelsea, jambo linalowafanya mashabiki kuwa na wasiwasi zaidi kuhusu uwezekano wa kumpoteza.

Enzo Fernandez Aelezeaa Mustakabali Wake Na Chelsea FC

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha Liam Rosenior amejaribu kupunguza presha kwa kusema hajayaona maoni ya mchezaji huyo, akisisitiza kuwa anajikita zaidi katika mechi zijazo za ligi. Lengo lake kubwa ni kuhakikisha Chelsea wanamaliza ndani ya nafasi nne za juu ili kurejea kwenye mashindano ya Ulaya.

Enzo Fernandez Aelezeaa Mustakabali Wake Na Chelsea FC

Kwa sasa, mustakabali wa Enzo Fernandez unabaki kuwa kitendawili. Ikiwa Chelsea watashindwa kufuzu mashindano ya Ulaya msimu ujao, uwezekano wa nyota huyo kuondoka utaongezeka maradufu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.