Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, ameandika historia mpya kwa kumpita Sir Alex Ferguson kwa idadi ya mechi alizosimamia kwenye UEFA Champions League. Hata hivyo, mafanikio hayo yamefunikwa na aibu ya kutolewa mapema baada ya kichapo cha jumla ya mabao 5-1 dhidi ya Real Madrid kwenye hatua ya 16 bora.

Katika mchezo huo, City walionekana kuzidiwa kila upande, huku Vinicius Junior akiwa mwiba mkali kwao. Baada ya ushindi wa 3-0 kwenye mchezo wa kwanza, Madrid walikamilisha kazi kwa ushindi wa 2-1, wakimaliza ndoto za City za kutetea heshima yao Ulaya. Bao la Erling Haaland halikuweza kubadilisha chochote, huku kadi nyekundu ya Bernardo Silva ikizidi kuwagharimu.
Pamoja na kipigo hicho, Guardiola amefikisha mechi 191 katika mashindano hayo, akimpita Ferguson aliyekuwa na mechi 190. Rekodi hiyo inaonyesha uimara na mafanikio ya muda mrefu ya kocha huyo katika klabu tofauti kama Barcelona, Bayern Munich na Manchester City.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Licha ya mafanikio hayo, bado Guardiola yupo nyuma ya Carlo Ancelotti ambaye anaongoza kwa mechi nyingi zaidi (218) na pia mataji mengi zaidi ya Champions League. Guardiola ana mataji matatu, sawa na makocha wakubwa kama Zinedine Zidane na Bob Paisley.

Kwa sasa, Manchester City wanakabiliwa na kipindi kigumu, wakipoteza mwelekeo hata kwenye ligi. Wakiwa nyuma ya Arsenal FC katika mbio za ubingwa, kikosi hicho kinahitaji kurejea haraka kwenye kiwango chao ili kuokoa msimu, huku wakijiandaa na fainali ya Kombe la Carabao pamoja na mechi muhimu za FA Cup.


