Tetesi za kiungo wa Chelsea, Enzo Fernández, kuhamia Real Madrid zimeanza kushika kasi, lakini ukweli ni kwamba bado hakuna uthibitisho rasmi wa dili hilo kufanyika. Kilichochochea moto zaidi ni kauli zake binafsi kuhusu mapenzi yake kwa jiji la Madrid.

Enzo amekiri wazi kuwa angependa kuishi Madrid, akilinganisha maisha ya huko na kwao Buenos Aires, kuanzia chakula hadi mazingira ya maisha. Kauli hizi zimewapa mashabiki na vyombo vya habari sababu ya kuamini kuwa anaweza kuwa na ndoto ya kuichezea Real Madrid siku moja.
Hata hivyo, kupenda kuishi Madrid si sawa na kuhamia Real Madrid. Kwa sasa, Enzo bado ana mkataba mrefu na Chelsea, na klabu hiyo ilitumia fedha nyingi kumsajili, hivyo haitakuwa rahisi kumuachia bila dau kubwa sana.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Pia, Real Madrid hawajaweka wazi kuwa wameanza mazungumzo rasmi ya kumsajili, licha ya kuhusishwa naye pamoja na Paris Saint-Germain. Kwa hiyo, taarifa zilizopo ni zaidi ya uvumi kuliko uhalisia wa haraka.

Kwa kifupi, Enzo anapenda mji wa Madrid, ana heshima kubwa sana kwa wachezaji wa Real Madrid kama Toni Kroos na Luka Modrić lakini hakuna uthibitisho kuwa anahamia Real Madrid kwa sasa. Dirisha la usajili likifunguka ndipo ukweli utajulikana ila kwa sasa, ni uzushi tu.

