Fenerbahce Wailaumu Al-Ittihad Kufeli Kwa Dili la Kante

Klabu ya Fenerbahce imeitupia lawama Al-Ittihad kwa kusababisha kushindikana kwa dili la kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, N’Golo Kante. Waturuki hao wamesema wazi kuwa wao walitimiza kila kipengele cha makubaliano, lakini uzembe wa upande wa pili ndio uliosababisha mpango mzima kuanguka dakika za mwisho za dirisha la usajili.

Kupitia taarifa rasmi, Fenerbahce wamesisitiza kuwa walikuwa wamefikia makubaliano kamili na wachezaji husika, katika dili lililomhusisha pia mshambuliaji wa Morocco, Youssef En-Nesyri, kuhamia Al-Ittihad. Zaidi ya hapo, walibainisha kuwa vipimo vya afya vya Kante vilifanyika kwa mafanikio na wao kama klabu walitekeleza wajibu wao kikamilifu na kwa wakati.

Fenerbahce Wailaumu Al-Ittihad Kufeli Kwa Dili la Kante

Hata hivyo, mambo yalibadilika ghafla. Fenerbahce wamedai kuwa Al-Ittihad waliingiza taarifa zisizo sahihi kwenye mfumo wa kimataifa wa usajili (Transfer Matching System), hali iliyosababisha dili hilo kushindwa kukamilika kabla ya dirisha kufungwa. “Tatizo hilo halikutokana na klabu yetu,” ilisema Fenerbahce, wakiongeza kuwa walichukua hatua zote muhimu kurekebisha hali hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa mujibu wa Fenerbahce, waliomba hata muda wa nyongeza na kufanya mazungumzo na FIFA ili kuokoa dili hilo. Lakini licha ya jitihada zote, wamesema Al-Ittihad hawakukamilisha taratibu zilizobaki bila kutoa sababu yoyote ya msingi. Matokeo yake, usajili wa Kante ukagota kabisa.

Fenerbahce Wailaumu Al-Ittihad Kufeli Kwa Dili la Kante

Kufeli kwa dili hilo kunakuja wakati Al-Ittihad wako kwenye kipindi cha mabadiliko makubwa, baada ya Karim Benzema kuondoka na kujiunga na wapinzani wao Al-Hilal. Ilionekana wazi En-Nesyri angeweza kuwa mbadala wake. Kwa sasa, mustakabali wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 unabaki kuwa kitendawili, huku Fenerbahce wakibaki na maswali mengi, na lawama nzito kwa Al-Ittihad.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.