Klabu ya Fenerbahce kutoka nchini Uturuki imefanikiwa kuinasa saini ya golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Croatia na klabu ya Dinamo Zagreb Dominik Livakovic.

Klabu ya Fenerbahce imeripotiwa kumalizana na golikipa Livakovic na golikipa huyo anatarajiwa kuwasili nchini Utruruki kwa saa 24 zijazo kwajili ya kuchukua vipimo vya afya na kukamilisha dili hilo jumla kuanza kuitumikia klabu hiyo ya Uturuki.FenerbahceMabingwa hao wa zamani wa ligi ya Uturuki wameonekana kuboresha kikosi chao kwa kiwango kikubwa wakitazamia kufanya vizuri katika msimu mpya wa ligi kuu ya Uturuki mwaka 2023/2024.

Klabu hiyo mpaka sasa imeshafanya maingizo kadhaa katika kikosi chake ambayo yanaonesha moja kwa moja kuna kitu kikubwa wamepanga kukifanya katika michuano mbalimbali ambayo watakua wanashiriki msimu huu.FenerbahceGolikipa Dominik Livakovic anaungana na wachezaji kama Eden Dzeko kutoka klabu ya Inter Milan ya Italia, Fred Rodrigues kutoka Manchester United na wachezaji wengine kadhaa kwajili ya kukijenga kikosi cha Fenerbahce msimu na kuhakikisha inakua moja ya timu tishio katika ligi kuu ya Uturuki.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa