Bernardo Silva Kusaini Mkataba Mpya Wiki Hii

Kiungo wa klabu ya Manchester City Bernardo Silva raia wa kimataifa wa Ureno anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa ulaya ndani ya wiki hii.

Bernardo Silva amekua akihusishwa kuondoka ndani ya klabu ya Manchester City kwa misimu kadhaa sasa na klabu ya Barcelona ikihusishwa zaidi, Lakini mpaka sasa hajaondoka na anatarajiwa kusaini kandarasi mpya wiki ambayo itaendelea kumuweka klabuni hapo zaidi.Bernardo SilvaKiungo huyo wa kimataifa wa Ureno amekua kwenye ubora mkubwa tangu ajiunge na Man City mwaka 2018 akitokea klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa, Huku akiwa moja ya wachezaji vipenzi vya mwalimu Pep Guardiola.

Kiungo huyo fundi alikua akiwaumiza vichwa mabosi wa Man City kutokana na sakata lake la kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo na mabingwa wa soka nchini Hispania klabu ya Barcelona wakitajwa zaidi lakini taarifa zinaeleza kiungo huyo amekubali kusaini mkataba mpya.Bernardo SilvaTaarifa za Bernardo Silva kukubali kusaini kandarasi mpya ndani ya klabu hiyo ni taarifa nzuri zaidi kwa klabu hiyo na mashabiki wake haswa kipindi hichi ambacho wamempoteza kiungo Ilkay Gundogan na kiungo Kevin de Bruyne kupata majeraha ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kidogo.

Acha ujumbe