Atamani Kibarua cha Madrid

Mourinho anatamani sana na haoni tatizo lolote hata kama leo hii akaitwa kuifundisha Madrid ambayo ana historia nayo tangu kipindi kirefu na anajua mambo yote yaliyopo ndani ya klabu hiyo. Wazo hilo limemjia baada ya kuulizwa anauonaje mwenendo wa sasa wa klabu yake hiyo ya zamani kuelekea mbio za kufukuzia mataji.

Taarifa zinazoendelea kuzagaa kwa sasa ni kwamba inawezekana Mourinho akawa ndio mrithi wa Solari ndani ya kikosi hicho ambacho hapo awali aliwahi kukihudumia kama nwalimu wa timu hiyo na kukiwezesha kupata mataji kadha wa kadha ambayo yalikijenga kikosi hicho na kukipa heshima kubwa hadi leo.

Wawili hao kwa sasa wanaweza kuwa mahala panapoendana kutokana na Mourinho kupoteza kazi ndani ya United na klabu yake hiyo ambayo aliwahi kuifunza hapo mwanzo kupoteza kabisa mwelekeo kwa sasa kwa hiyo wote hao kwa sasa wana majanga makubwa ya kuhangaika kurejesha heshima zao ambazo zimepotea kwa kipindi hiki.

Solari aliichukua Madrid iliyokuwa chini ya Lopetegui hapo awali kutokana na mwalimu huyo kushindwa kufanya kile ambacho wamiliki wa klabu hiyo walitegemea kukipata kutoka kwake. Hivyo, ili kunusuru hali mbaya iliyokuwa ikiendelea kikosini hapo iliwalazimu kutafuta mbadala wake ambao kwa hakika kuna baadhi ya mabadiliko yameonekana kwa sasa.

Vichapo vitatu mbele ya Barcelona vimeibua hisia mpya endapo Solari akipewa kikosi hicho kama ataweza kukimudu lakini wengi wanaona kwamba kwa hali ilivyo sasa ataweza kuelemewa na kikosi hicho na itakuwa vigumu kwake kupata matokeo ya tofauti hivyo wanamwona kama hawezi kuwa chaguo sahihi kuongoza kikosi hicho kwa sababu matokeo ya awali yanaonesha baadaye yake ipoje.

Mourinho, aliyeshinda La Liga na klabu hiyo, Copa del Rey na Super Copa de Espana katika miaka yake mitatu ndani ya ligi hiyo ya Hispania, anaonekana kwa sasa kufunguliwa milango ya kujiunga na miamba hao ili aweze kuhudumu kutokana na historia kubwa aliyonayo na uwezo wake ambao hakika sio wa kubezwa.

Hata baada ya kuulizwa kama angeweza kuwa tayari kujiunga na klabu ambayo aliwahi kuhudumu hapo awali amelijibu bila wasiwasi swali hilo ya kwamba kwake hana tatizo yupo tayari kujiunga wakati wowote na hana pingamizi yoyote kama akipata nafasi ya kuifundisha klabu ya namna hiyo.

Kwake ni ufahari mkubwa kuona timu ambayo uliifundisha awali bado inajali na kuheshimu nafasi yake ndani ya kikosi chao na anaona ni heshima kubwa sana kwake maana ni wachache sana hupewa heshima ya namna hiyo. Muda utasema!

Makala ijayo

6 Komentara

    Taarifa nzur

    Jibu

    Mourinho anaipenda sana Madrid na Manchester #Meridianbettz

    Jibu

    Ni vizur usisahau ulipotoka

    Jibu

    Duuh jamaa anaikubali sana madrid

    Jibu

    Mourinhno ni kocha hanayejielewa sana

    Jibu

    Mourinho sio kocha mzuri

    Jibu

Acha ujumbe