BALLON D'OR: Ndoto na Tamaa Mane Kua George Weah wa Pili

Huhitaji kuwa mtu bora ili ufanye vitu bora ila zaidi unahitaji kufanya vitu bora ili uwe mtu bora, George Weah ni mwafrika pekee aliyebeba tuzo ya ballon dor mpaka sasa, ilikua mwaka 1995 ulimwengu ulisimama ukampatia tuzo yake. Ulisimama kwa sababu ya ubora wake katika kufunga alimaliza kama mfungaji bora wa klabu bingwa ulaya akiwa na klabu yake ya Paris st german waliyoishia katika hatua ya nusu fainali, huku magoli ya George weah pia yakiwafanya wabebe kombe la ligi kuu Ufaransa akahamia Ac Milan nako akawa moto katika kufunga

George Weah alitengeneza ubora wake katika kufunga, sehemu aliyoamini ndiyo ingemfanya aonekane kuwa bora, na kweli ikamfanya kuwa bora, dunia ikamtambua kama mchezaji bora wa dunia. Magoli kwa kiasi kikubwa ndiyo yanayoonekana alama ya mchezaji bora, macho ya soka yanatazama sana washambuliaji kuliko kazi ngumu inayofanywa na makipa ama kazi ya roho ya paka inayofanywa na viungo.

Kushinda ballon dor bila kuwa na magoli mengi si kazi nyepesi unahitaji uishawishi dunia kwa uwezo wa ajabu sana kuisaidia timu kubeba mataji haitoshi kukufanya uonekane mchezaji bora wa dunia.

Luka Modric mwaka 2018 alifanya kazi ngumu sana na ya kipekee, akabeba ubingwa wa ulaya na Real Madrid kwa pasi zake zilizopakwa sanitizer, pia akaipeleka Croatia fainali kombe la dunia. Dunia ingepewa dhambi kama wasingempa tuzo, unataka nini ya hicho, magoli ya Messi na Ronaldo yakafanywa kafara kwa muda jamaa akapewa tuzo yake.

Sadio Mane

Miaka 25 imepita mpaka sasa tangia George Weah atwae tuzo hiyo hakuna mwaafrika mwingine aliyebeba tuzo hiyo, wamepita waafrika wengi Samuel Eto, Didier Drogba bado hawajaishawishi dunia kupewa tuzo hiyo, kwa sasa Sadio Mane anapitia mtihani huo mzito anapiga kazi ngumu sana Liverpool. Mwaka jana alisaidia Liverpool kubeba ubingwa wa uefa na kumaliza nafasi ya pili, lakini dunia haikuona kama ilitosha kumpa tuzo ya ballon dor, machozi yake yakaenda na maji.

Kabla ya kutazama ubora wake walitazama kwanza vitu bora alivyofanya wakaona hana magoli mengi, pasi za mwisho alizotoa si nyingi sana kwao ikawa rahisi kumfanya asiwe mshindi wa ballon dor. Mane anahitaji kufanya vitu kama alivyofanya George Weah kushinda tuzo hiyo, kufunga magoli ya kutosha, huku timu yake ikifanya vizuri, jicho la ballon dor linaweza kumtizama kirahisi, nje ya hapo unahitaji kufanya vitu vigumu sana kupewa tuzo hiyo.

George Weah alitambua hilo, yeye akachagua kufunga sana, jay jay okocha alikua sanaa ya utumbuizaji uwanjani dunia ikazima taa kabisa huku ikifurahia burudani yake. Sadio Mane anakazi ngumu sana, kuchagua kuwa George Weah wa pili, ama acheze soka la kufikirika walilocheza wakina Luka Modric, Ricardo kaka kupewa tuzo hiyo.

7 Komentara

    Wachezaji wengi wa Africa wanashiba sifa wanabdi waongeze juhudi

    Jibu

    Wachezaji wa africa hawapewi kipaumbele wanachostahili sadio mane anajituma sana na ni mchezaji bora zaidi

    Jibu

    Anastahilii kupewa sifa zake na hongera

    Jibu

    sadio mane ni mchezaji mzuri ila anapenda sana kujidondosha dondosha

    Jibu

    Waafrika wanatakiwa waongeze juhudi

    Jibu

    africa hawapewi kipaumbele wanachostahili sadio mane anajituma sana na ni mchezaji bora zaidi

    Jibu

    Mm nashangaa sana sijui ngozi zetu ndio sabab hatupewi kipaumbele maana kama tuzo msimu wa 2019 sadio mane alistahili kupewa kwa mambo makubwa aliyo fanya pamoja n timu yake alipo ifikisha ila wamekua na upendeo sana kumuangalia tuu messi messi basi bila kuangalia alie jitahid kwa msimu husika ndio maana Ronaldo alisusaga mambo kama haya wala hakwenda kuhudhuria ugawaji wa tuzo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.