PSG Kutwaa Ligue 1 Kunawapa Matumaini Liverpool?

Paris Saint Germain wamepewa ubingwa wa Ligi ya Ufaransa, League 1 kufuatia maamuzi wa kumaliza msimu wa ligi kutokana na janga la virusi vya corona lililoathri muendelezo wa michezo mingi ulimwenguni.

Ligi Kuu ya Uingereza, EPL bado kuna matumaini kuwa huenda msimu ukaendelea kwa sehemu ya mechi ambazo zimesalia wakati Liverpool wakiwa vinara wa ligi, maamuzi ya kumaliza msimu hayakuungwa mkono na watu wengi.

Liverpool wanaweza kuanza kuhisi kuona mwanga wa matumaini ikiwa msimu wa EPL nao utaamua kumalizika na vigezo kama vilivyotumia kuwapa taji PSG vikatumika EPL.

Mpaka sasa waendeshaji na vilabu vya EPL vinaendelea kutekeleza ushauri wa wataalamu na kushauriana zaidi kuhusu msimamo wao wa kumaliza ligi kwa kucheza mechi zilizosalia. Uwezekano mkubwa unaopigiwa upatu na kufanyiwa mipango zaidi ni kucheza mechi bila mashabiki na wachezaji kuwekwa karantini kabla ya kukutana michezoni.

PSG walikuwa wanaongoza kwa pointi 12 zaidi ya Marseille ambao walikuwa wamekalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi. Maamuzi ya serikali kuwa ligi imalizike, yamawapa PSG taji la League 1 kwa msimu wa 2019-20.

Hata hivyo kuna changamoto, na bado haijaweka wazi kama kuna vilabu ambavyo vitashuka daraja. PSG wamekusaja taji la 3 mfululizo na wanatarajia kupata nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa.

Liverpool wanaongoza kwa pointi 23 mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City. Kulikuwa na hofu kuwa ikiwa msimu utamalizika huenda matumaini ya Liverpool juu ya kutwaa taji yakapotea! Lakini PSG wametoa mwanga kwa majogoo!

10 Komentara

    England mpaka kieleweke hakuna kulala

    Jibu

    PSG mko juu

    Jibu

    Liverpool tupo juu

    Jibu

    Vizur sana

    Jibu

    Psg bora wapewe ubingwa

    Jibu

    Ushindiii ni lazimaaa

    Jibu

    Liverpool ushindi lazima bana

    Jibu

    Corona inafanya vbaya kwa wapenda kabumbu

    Jibu

    Wapambane ubingwa wamezani wasahau

    Jibu

    Liver pool wapew tu

    Jibu

Acha ujumbe