De Ligt: Najifunza Kutoka Hapa Juventus

Matthijs de Ligt anasema anajaribu kujifunza kutoka kwa wanatimu wenzake wa Juventus, Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini.

Kinda huyu mwenye miaka 20 ameweka wazi kuwa mwanzoni halikuwa lengo lake kucheza kama mlinzi. De Ligt alifika Juventus msimu wa joto uliopita akitokea Ajax kwa paundi milioni 85.

Tangia kufika klabuni hapo anasema anajifunza mambo mengi zaidi na kuendelea kujiboresha. Amebainisha kuwa katika vitu vingine vingi, kujitambua kwake imekuwa nguzo ya mafanikio, na anaamini hii itampigisha hatua ndefu zaidi.

“Ni vyema kujitamba mwenyewe kama akili yako iko sawa. Kama uko tayari, hakuna anayeweza kukuzuia” Aliliambia jarida la Champions Journal.

Kama mlinzi makini, alihitaji kujua ni mambo gani mazuri ayafanye, na kurejea nyuma kujifunza kupitia makosa, na hufanya hivyo mara nyingi.

Licha ya kuwa na umri mdogo tayari kinda huyu ameshacheza na mastaa wengi wakubwa, kwa nafasi yake wakiwepo akina Virgil van Dijk kwa Netherlands, pamoja na Bonucci na Chiellini hapo Juventus.

Hadi alipokuwa na umri wa miaka 15, De Ligt alikuwa anacheza kama kiungo mshambuliaji hadi aliposhauriwa kubadilisha nafasi hiyo.

“Nilicheza sana kama kiungo, nilifunga magoli, nilitoa asisti, na ghafla wakaniambia kuwa ingekuwa vyema kwa kazi yangu ningeenda nafasi ya ulinzi, katikati.”

Wenyewe wanasema mipango siyo matumizi! Staa huyu anafurahia nafasi yake kwa sasa kama mlinzi na anaendelea kujifunza mengi licha ya ukweli kwamba hakuwahi kuwaza hivyo awali.

3 Komentara

    ktk soka mwalimu ndo uwa anaweza kuona mbali uenda ktk safu ya ulinzi utafanya vyema zaidi

    Jibu

    Matthijs de Ligt Jicho lengine kwenye ulimwengu wa Soka!!!!

    Jibu

    Beki kisiki huyo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.