Barca: Hatuna Mazungumzo Kumuuza Rakitic

Paris Saint-German wanamtamani mchezaji wa Barcelona bwana Ivan Rakitic lakini Barcelona kwa sasa hawataki kufanya mazungumzo juu ya kumuuza mchezaji huyo ambaye PSG wameonyesha kumuhitaji wakati thamani yake kwa sasa ikitajwa kuwa Euro milioni 125.

Kocha mkuu bwana Ernesto Valverde anamchukulia Rakitic kama mmoja wa wachezaji muhimu zaidi kwa timu hiyo ambaye asingependa kusikia hadithi za kuondoka kwake.

Hata hivyo Paris Saint-German bado wanaweza kuwa na nafasi ya kumnyakua staa huyo ikiwa watakubali kumlipia gharama ya kuvunja mkataba wake kwa kuwa hakutakuwa na kikwazo tena kuwazuia timu hiyo kumnasa Rakitic. kwa sasa Ivan Rakitic mwenye umri wa miaka 30 ataendelea kuwepo barcelona mpaka itakapoamuliwa tofauti na uongozi wa barca.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.