Wakala wa mchezaji Paul Pogba bwana Mino Raniola amemtolea uvivu aliyekuwa mchezaji wa Man utd Paul Scholes juu ya madai dhidi ya mteja wake kufuatia Kiwango anacho onesha katika timu hiyo hasa siku ya jumapili pale Brighton ambapo Man Utd walipoteza kwa kupigwa bao 3-2.
kwa mujibu wa mchezaji huyo wa zamani anadai pogba alikuwa na mchezo mbaya na pia hakua kiongozi katika mechi waliyopoteza jumapili kwenye ligi ya Primier.
Hata hivyo Mino Raniola anadai Scholes asingeweza kumtambua kiongozi kama angekuwa mbele ya sir Winston Churchill, aliongeza kuwa kuna watu ambao wanalazimika kuongea ili wasisahaulike likiwa ni dongo kwa Scholes. Raniola alisisitiza kuwa kulikuwa na mapungufu katika uongozi na ndio maana Pogba akaonekana ndio chaguo sahihi. Lakini Pogba mwenyewe alikiri mapungufu yake hasa katika mchezo wa Brighton.


Furahav
Mmh majanga.
Gabriel
Yuko sahihi kabisa