Tuchel Athibitisha Bayern Wanahitaji Mshambuliaji

Kocha wa klabu ya Fc Bayern Munich Thomas Tuchel amethibitisha klabu yake inahitaji mshambuliaji mwenye kiwango cha dunia kutokana na kauli ambayo ameitoa mapema leo akizungumza na wanahabari.

Kocha Tuchel amesema kua klabu zote ambazo zinatawala kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya zina mshambuliaji wa kiwango cha dunia, Hivo kila timu inahitaji mshambuliaji wa aina hiyo ni wazi kauli hiyo inaonesha Bayern wataingia sokoni kutafuta mshambuliaji kwenye dirisha kubwa.TuchelKlabu ya Bayern Munich imekua ikipitia wakati mgumu katika safu yake ya ushambuliaji kutokana na kukosa mshambuliaji mwenye uwezo wa juu, Hiyo ni baada ya kuondokewa na mshambuliaji wao Roberto Lewandowski kwenye dirisha kubwa lililopita akitimkia kwa miamba ya soka nchini Hispania klabu ya F Barcelona.

Kocha Thomas Tuchel ambaye amepewa mwezi mmoja uliopita akichukua timu kutoka kwa Julian Nagelsman alieondolewa klabuni hapo ameonesha nia ya kuingia sokoni na kutafuta mshambuliaji wa kiwango cha dunia ili waweze kuleta ushindani kwenye michuano ya ulaya mwakani ambapo mwaka huu walitupwa nje hatua ya robo fainali.TuchelBayern Munich wanahusishwa sana mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Kane ambaye inaelezwa ndio wanamuona kama mbadala sahihi wa Lewndowski kwakua ana ubora ambao anauhitaji, Lakini changamoto ni kua je mchezaji huyo anaweza kukubali kutoka nje ya Uingereza.

Acha ujumbe