Wakati Argentina wanapewa uenyeji wa Kombe la dunia 1978 walihitaji utulivu mkubwa kwenye Jiji la Buenos Aires, ndipo Dikteta Juan Carlos Ongania aliagiza maskini wote watolewe katikati ya jiji na kupelekwa Barrio Ejercito do Los Andes ‘Fuerte Apache’ mnamo 1966

Miaka 18 baadae tarehe 5 mwezi wa 2 anazaliwa Carlos Alberto Martinez baadae anabadili jina na kuitwa Carlos Tevez kuepusha ugomvi kati ya klabu, Old Boys na Boca Juniors, alizaliwa kwenye mitaa ya Ciudadela ila alienda kulelewa na Mama yake mkubwa, Adriena Naoemi Martinez
Ambapo katika maeneo ya Fuerte Apache Tevez alijifunza uhuni, udokozi na ukorofi, kila aina ya matukio mabaya yalipatikana Fuerte Apache, ilipelekea Tevez kuvunja meno yake ya mbele na kumwagiwa maji kupelekea kovu analodumu nalo maishani mwake, Tevez alikua kichwa ngumu kiasi cha shangazi yake kutaka kumrudisha kwa wazazi wake lakini alisha chelewa.
Kovu la Tevez linaakisi maisha halisi ya watu wa Apache, Watabibu walimwambia Tevez inawezekana kufuta kuvu lako la usoni lakini Tevez aligoma kufanyiwa upasuaji wakutoa kovu, aliamini ni alama yake kutokea mitaa iliyomlea ya hukoFuerte Apache.
Tevez aliliteka soka la Amerika Kusini, Boca Juniors, Corinthians na baadae barani Ulaya pale West Ham, Manchester United na City kisha Juventus, Tevez huyu aliwahi kufunga goli pale Etihad kisha akavua jezi kuonesha jina FUERTE APACHE, ni Tevez huyu aliyesepa Ulaya kurejea Boca Juniors ili awe karibu na Fuerte Apache

Vijana wa mtaani kwao wakampachika jina El Apache ,yani yeye ndio alama ya mtaa wao ni Tevez mtu muhimu kwao na nembo yao licha ya dharau za Dikteta Ongania na taswira ya Apache kwa kipindi hicho.
Ufikapo Fuerte Apache usimtaje Lionel Messi wa Rosario, wao Mfalme wao ni Tevez aliyekuwa kwa moshi wa sigara, ufikapo Apache hisi upo Bogotá Columbia, Santiago Chile na Montevideo pale Uruguay, watu wa Apache wana style zao na utamaduni wao.


Ester jackson
Hakuna MTU asiye kubalika kwao
Rehema Dickson
Ni vizuri kukubarika kafanya mambo mengi na yakupendeza anastahili kukubarika kwao
Furahav
Ametisha Tevezi.