Chelsea: Gilmour Anaota Kukimbiza Duniani

Kinda wa Chelsea Billy Gilmour mwenye miaka 17 anasema anataka kuwa mchezaji bora zaidi Duniani. Gilmour alijiunga na Chelsea akiwa na miaka 16 mwaka 2017 kwenye kikosi cha vijana wa chini ya miaka 18, mwezi Julai 2018 amejiunga na kikosi cha vijana wa chini ya miaka 23.

Gilmour ameanza kung’ara katika midani za kimataifa anatazamiwa kuja kuwa mchezaji mkubwa sana baadae. Nafasi yake uwanjani ni kiungo, akiwa na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 amefunga magoli 8 katika gemu 21 alizocheza. Kikosi cha vijana wenye umri wa miaka chini ya 23 amefunga goli mara moja na kutoa pasi 2 za magoli.

Kinda huyu alizungumza na chanzo cha habari Daily Mail akasema “Hii ndio hamu yangu ya wakati wote, kuwa bora duniani, kama kuna mtu ni bora zaidi yangu mimi nataka kuwa bora zaidi yao! nachukia sana kushindwa na mda wote nimekuwa nikifikiria ushinndi.” anasisitiza yuko tayari kufanya jitihada ili aweze kuiishi ndoto yake hiyo ya kuwa mwansoka bora duniani.

2 Komentara

    Dogo yupo vzr sana

    Jibu

    Pambana utimize ndoto zako.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.