Kolo Muani: Siondoki PSG Januari

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayekipa ndani ya klabu ya PSG Kolo Muani ameweka wazi juu ya tetesi zinazomhusisha yeye kutimka klabuni hapo majira ya baridi mwezi Januari.

Kolo Muani ameweka wazi hana mpango wa kuondoka ndani ya klabu ya PSG na badala yake ataendelea kupigania nembo ya klabu hiyo, Hii imekuja baada ya tetesi kuenea kua mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Frankfurt ya nchini Ujerumani anatamka kutimka ndani ya viunga vya Parc de Princes.kolo muaniMshambuliaji huyo amekua sio kipaumbele kwenye kikosi cha PSG chini ya kocha Luis Enrique jambo ambalo limefanya tetesi za yeye kutimka kuibuka, Kwani wamehusisha na hali yake klabuni hapo na huenda hana furaha na ndio sababu ya kutaka kuondoka lakini yeye mwenyewe amekanusha taarifa hizo.

Klabu ya PSG itaendelea kusalia na Kolo Muani kwani mshambuliaji huyo ana mkataba bado na mabingwa hao wa Ufaransa na ameonesha hana nia ya kuondoka klabuni hapo kama alivyoeleza yeye mwenyewe, Hivo kwa timu ambazo zilianza kumtolea machjo mchezaji huyo zitambue kua mshambuliaji huyo akili yake inaiwaza PSG tu.

Acha ujumbe