Mendy Arejea Uwanjani Asaini Lorient

Aliyekua beki wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ufaransa Benjamin Mendy amefanikiwa kurudi uwanjani na amejiunga na klabu ya Lorient ya nchini Ufaransa.

Benjamin Mendy ambaye alikua anakabiliwa na kesi za ubakaji na kumueka nje kwa muda wa miaka miwili na nusu, Lakini alifanikiwa kushinda kesi zake na sasa atarejea uwanjani rasmi na atajiunga na klabu hiyo kutoka nchini Ufaransa.mendyBeki huyo alithibitishwa na mahakama kushinda kesi zake zilizokua zinamkabili na kukutwa hana hatia wiki iliyomalizika, Hivo kumueka mchezaji huyo huru na kuweza kurudi dimbani kuanza kucheza mpira kwa mara nyingine.

Benjamin Mendy amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Lorient hivo atakua klabuni hapo mpaka mwaka 2025, Hii inaweza kua fursa kwa beki huyo kuonesha uwezo na kuweza kurejea kwenye vilabu vikubwa kwa mara nyingine.mendyBeki Mendy alikua moja ya wachezaji wazuri wenye ubora mkubwa kwenye kikosi cha Monaco kabla ya kujiunga na Man City mwaka 2017 ambapo ndipo alipokumbwa na kashfa ya ubakaji ambazo zilimueka nje ya uwanja mpaka wiki iliyomalizika.

Acha ujumbe