Gaucho Anamkubali Nani: Lionel Messi au Cr7?

Kwenye mahojiano ambayo staa wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Ronaldinho Gaucho ameyafanya na jarida la SPORTS la huko Hispania ameongelea mambo mengi kuhusu kabumbu la wakati huu.

Moja ya mambo ambayo Dinho amesema ni kwanza mchezaji ambaye anatamani angecheza naye katika kipindi chake ila hakucheza naye kwa wakati huo ambapo amemtaja kiungo wa klabu ya Barcelona, Phellipe Coutinho kama kiungo ambaye angefanya mchezo wa kandanda kuwa rahisi kwake kama wangecheza pamoja dimbani!

Mtabe huyo wa soka anaamini kwamba Iniesta na Coutinho ni kati ya viungo bora sana ambao amewahi kuwaona katika soka na Coutinho atakuja kuwa moja katika ya wachezaji wakubwa sana duniani siku za mbeleni.

Swali gumu!

Ila mtangazaji aliamua kumuuliza Ronaldinho swali ambalo pengine kila mtu wa kandanda amewahi kuulizwa ama kuuliza kwamba Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ni yupi anamkubali zaidi? “Mimi sipendi swali hili ila ukiwaangalia hawa wawili mimi navutiwa zaidi na namna Lionel Messi anavyocheza.”

Ronaldinho amesema kwamba Cristiano Ronaldo ni mchezaji ambaye amekamilika na ana kila kitu awapo dimbani kama ilivyo kwa Lionel Messi ila bado yeye anamuona Messi anavutia zaidi kumtazama akicheza.

3 Komentara

    ni mchezaji ambaye amekamilika na ana kila kitu awapo dimbani

    Jibu

    Ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Dinho yupo sahihi la pruga messi ni noma

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.