Kiungo wa Liverpool Jordan Henderson, mwenye miaka 28 ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu kwenye Kombe la Dunia katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza anasema kichapo walichokipata dhidi ya Croatia katika nusu fainali ya Kombe la Dunia kitakua kama muongozo wa jitihada zao za ushindi katika ligi ya mataifa inayofahamika kama UEFA Nations League.
Uingereza wanatarajia kukutana na Uhispania kwenye dimba la Wembley Jumamosi September 8, 2018. Hii itakuwa ni gemu yao ya kwanza tangu walipopoteza gemu dhidi ya Croatia kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia. Baada ya gemu hii wataelekea katika dimba la Leicester la Nguvu ya Mfale (Kings Power) kucheza gemu ya kirafiki dhidi ya Switzerland.
Henderson ambaye amecheza mechi 44 za kimataifa, aliwataka wachezaji wenzie watumie uzoefu wa kombe la dunia kupata mzuka wa gemu walizonazo mbele yao ili wawe bora zaidi. “tunawachezaji wengi vijana katika timu tunaweza kujifunza kupitia kombe la dunia ili kuwa bora zaidi, uzoefu ule hautaweza kupotea kwangu mimi hata kwa wanzangu” -Henderson.
Henderson anaamini taifa linaisapoti timu yao ambayo inaundwa na vijana wengi, katika fainali za kombe la dunia ilikuwa nafasi ya tatu ikiundwa na vijana wenye wastani wa umri wa miaka 26 kwa jumla. Uingereza wanatarajia kichapo dhidi ya Croatia kiwe fundisho katika gemu wanazoenda kucheza.


Furahav
Waingereza wanazingua sana.
devotha
asante kwa habari